Msafara wa Dr. Slaa ukiwasili uwanjani
Dr. Slaa na Senator Shelby wakibadilishana mawazo wakielekea uwanjani
Watu wa kila aina mashuhuri walifika kumsalimia Dr. Slaa
Dr. Slaa na Mkewe wakilakiwa na Rais wa Chuo
Watoto nao walijitokeza kumsalimia na kupiga picha na mgeni mashuhuri Dr. Slaa
Dr. Slaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi ya Masenators walioalikwa kujumuika naye
Moja ya Viongozi wa Juu Nchini Marekani
Moja wa mamea mashuhuri marekani akimsalimia Dr. Slaa
Dr. Slaa akikaribishwa Ukumbuni kwenye Chakula cha Asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake
Watu wengi mashuhuri walioalikwa walimiminika kusalimiana na Dr. Slaa
Uwanja ulijaa hasa. Watu zaidi ya laki moja walihudhuria
wakiwa katika chumba cha watu mashuhuri. Baadhi ya watu mahuhuri kama yeye hawakujizuia kwenda kumsalimia. Akifungua mchezo wa leo, Dr. Slaa alirushwa moja kwa moja na moja ya luninga kubwa zaidi nchini marekani
Dr. Slaa na Gavana
Viongozi Mashuhuri wakiwa uwanjani kabla ya mchezo kuanza. Dr. Slaa ndiye mgeni Rasmi. Hapa ni chumba maalum cha rais kwa ajili ya wageni mashuhuri
Mshindi wa Nobel Peace Price na Dr. Slaa ndani ya Chumba cha watu mashuhuri wakijadili neno
Dr. Slaa akisalimiwa na mmoja wa US congressmen waliohudhuria mchezo
Ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa kiafrika kupewa mapokezi makubwa
ambayo Dr. Slaa ameyapokea katika ufunguzi wa mchezo wa mpira maarufu
kama football. Dr. Slaa alialikwa na Chancellor pamoja na Rais wa chuo
kikuu cha Alabama kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo baina ya Alabama na
Georgia State. Kiongozi huyo wa Chadema alipokewa na viongozi wa ngazi
mbali mbali wa kitaifa na wa jimbo la Alabama. Akimkaribisha Dr. Slaa
katika chakula cha asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake, Chancellor wa
chuo hicho, amemfananisha Dr. Slaa na Nelson Mandela kutokana na juhudi
zake za kupambana ufisadi nchini Tanzania. “Tunajua jinsi polisi
wanavyowaua raia na kuwakamata wapinzani” alisema kiongozi huyo.
Kadhalika kiongozi huyo amemsifu Dr. Slaa kutokana na msimamo wake, sera
zake za kulikomboa Tanzania kutoka katika umasikini licha ya chama
chake kutungiwa kesi za ughaidi.
Kwa upande wake, wakiwa kama moja ya vyuo vikuu nchini marekani, wako tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Dr. Slaa hasa katika sekta ya elimu. Wamemuomba ajisikie nyumbani na kufurahia mchezo wa American football. Kwa unyenyekevu Dr. Slaa aliwashukuru governor, na viongozi wengine kwa kuwa wakarimu sana kwake na mkewe na watu wa Tanzania. Amefurahishwa jinsi wamarekani wanavyokuwa na hamasa na kuipa kipaumbele michezo. Nimejifunza kwamba michezo ni moja ya mbinu ya kuiunganisha taifa hasa tunapokuwa na changamoto nyingi kama za kwetu alisema Dr. Slaa. Kadhalika amesema kwamba, chama chake cha Chadema ina sera ya kukuza vipaji kupitia taasisi za michezo nchini Tanzania na siyo kuwaleta Makocha wa kigeni, mmoja baada ya mwingine na kuwapeleka Ikulu kula pilau na kupiga picha. Nilichojifunza ni kwamba, lazima nirudi na ujumbe kwa watanzania kuweka mifumo endelevu ya michezo kuanzia shule za misingi hadi vyuoni. Nilichoona hapa ni mfano wa kuigwa alimalizia Dr. Slaa.
http://chademadiaspora.blogspot.com/2013/10/dr-slaa-apokewa-kifalme-nchini-marekani.html