http://kariakoodsm.blogspot.com
KARIAKOO BLOG:Kwa Habari Kali Za Mjini | SIASA | BURUDANI | UCHUMI | FASHION | BLOGGER TRICKS | UDAKU | MICHEZO | WASILIANA NA MIMI|0713305567 |urassaombeni@yahoo.com|KWA| MATANGAZO| BABARI| USISITE PIA KUCOMMENT KWENYE HABARI ZETU | <div style='background-color: #de24de;'><a href='http://www.ikiloop.com/' title='link'></a></div>

RASIMU YA KATIBA MPYA TANZANIA IKO HAPA...

Kupata rasimu ya katiba mpya ya Tanzania bofya HAPA

RIPOTI ILIYOWANG'OA MAWAZIRI WA 4 HII HAPA:

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA KUHUSU TATHMINI YA MATATIZO YALIYOTOKANA NA OPARESHENI TOKOMEZA ;


1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, wakati Bunge likijadili hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo muhimu la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2013, iliyowasilishwa na Mhe. Said Nkumba, Mbunge wa Sikonge kuhusu Mgogoro kati ya Wafugaji na Wakulima, Hifadhi na Uwekezaji, Mheshimiwa Spika alitoa Uamuzi ‘Speakers Ruling’ kuwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ishughulikie kazi ya kutathmini na kuangalia jinsi Mpango wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na kutekelezwa na Serikali kupitia ‘Operesheni Tokomeza’.

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MWANZA AUWAWA KWA KUPIGWA MAWE.


Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini Mwanza.

Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wananchi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani? 

Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani. Kwa mujibu wa Katibu wa CCM ndg Joyce Masunga (maarufu kama Maziwa Fresh) ni kweli kuwa tukio hili limetokea na tunaendelea kufuatilia kupata habari zaidi.


Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kushambuliwa 



Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa Bungando

PICHA :FOLENI KUBWA YA KWENDA KUAGA MWILI WA MAREHEMU NELSON MANDELA LEO


















Zitto, Lema, Werema watifuana


SAKATA la mabilioni yanayodaiwa kufichwa na Watanzania nje ya nchi jana lilileta zogo bungeni baada ya Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema, kutifuana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, huku Mbunge wa Arusha Godbless akiwataka wote wawili wampe majina ayataje hadharani kama wanashikwa na woga.

Huku Zitto akisisitiza kuwa serikali haionyeshi nia ya kuwachukulia hatua walioficha pesa hizo nje ya nchi, Jaji Werema aliliambia Bunge kuwa Zitto mwenyewe ameshakiri chini ya kiapo ofisini kwake kwamba hana majina wala akaunti za watu hao, kinyume cha kauli yake huko nyuma alipowahi kusema kuwa anawajua.

Kwa mujibu wa Jaji Werema, kwa kuwa sakata hili liliibuliwa bungeni na Zitto, serikali iliunda kamati malumu ikitarajia kuwa mbunge huyo ndiye angetoa ushirikiano kurahisisha uchunguzi huo, lakini mara zote amekuwa akiikwepa kamati.

Alisema Zitto anapotosha Bunge na taifa kuhusu sakata hilo. Kauli ya Werema ilitolewa jioni wakati Bunge limekaa kama kamati, akijibu hoja ya Zitto aliyoitoa asubuhi akiishutumu serikali kwa kutokuwa na nia thabiti ya kufuatilia pesa hizo ili zirejeshwe.

Lakini kabla ya Mwanasheria Mkuu kujibu, Lema alikuwa amewataka serikali na Zitto kuacha kuchezea akili za Watanzania; kwamba wawe na ujasiri wa kutaja wahusika badala ya kupiga danadana.

Picha 60 kutoka kwenye misa ya kumuombea hayati Nelson Mandela


Marais zaidi ya 100 wahudhuria Afrika kusini kuuaga mwili wa NELSON MANDELA...!!


Hizi ni picha mbalimbali toka SA wakati wa kuuaga mwili wa mzee Mandela




Source: BBC

ShareThis