![]() |
Leodger Tenga Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu aliyemaliza muda wake akimkabidhi Mpira Jamal Malinzi Rais Mpya wa shirikisho hilo mara baada ya kumshinda mpinzani wake aliyekuwa makamu wa Kwanza wa shirikisho hilo Bw. Athman Nyamlani kwa kura 73 kwenye uchaguzi ulifanyika katika ukumbi wa Water Front jijini Dar es salaam na kumalizika usiku huu, Katika uchaguzi huo Mgombea wa umakamu wa wa rais Walace Karia amefanikiwa kuwashinda wapinzania wake Imani Madega na Ramadhan Nassib |
![]() |
Leodger Tenga Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu aliyemaliza muda wake akizungumza na kumpongeza Jamal Malinzi Rais Mpya wa shirikisho |
![]() |
Baadhi ya wafuasi wa Rais Mpya wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Bw. Jamal Malinzi wakishangilia na kupongezana mara baada ya kusikia matokeo ya uchaguzi huo yakionyesha Jamal Malinzi ameshinda. |
![]() |
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji Bw. Mvela kutoka Iringa hali ilibadilika kutokana na furaha jambo lililopelekea kupata mshtuko hapa akisaidiwa kutolewa nje ya ukumbi na wajumbe wenzake. |
![]() |
Kutoka kulia ni Leodger Tenga Rais wa TFF aliyemaliza muda wake mwakilishi wa FIFA Ashford Mamelodi na Henry Tandau wakiwa katika chumba cha uchaguzi huo. |
![]() |
Jamal Malinzi Rais Mpya wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF akimpongeza makamu wake wa Rais Bw. Wallace Karia mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo. |
.
PICHA NA KUKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE WATER FRONT DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment