serikali ililifungia gazeti la wiki la MwanaHalisi ambalo lilichapisha kwa undani taarifa za ofisa wa usalama aliyetajwa na Ulimboka, likidaiwa kuwa linachochea. Ahadi ya Kova kuwasaka wahusika na kuwachukulia hatua ili kuhakikisha tukio hilo halijirudii tena imeshindikana kutekelezeka kwani usiku wa Machi 6, mwaka huu, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini, Absalom Kibanda, naye alitendewa unyama kama wa Dk. Ulimboka. Kova aliunda kikosi kazi kingine kuchunguza tukio hilo lakini hadi leo hakuna ripoti iliyotolewa. Waliomteka na kumtesa Kibanda bado hawajulikani na siku zinazidi kwenda. Katika kudhihirisha kuwa polisi walikurupuka na kumshtaki Mulundi ili kuwaziba wabunge midomo wasijadili suala hilo bungeni, juzi Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), aliifuta kesi hiyo dhidi ya raia huyo wa Kenya. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama likiwamo Jeshi la Polisi, wanalipwa mshahara kutokana na kodi za wananchi ili wafanye kazi zao kwa weledi na ufasaha, kwanini washindwe kuwabaini waliowateka na kuwatesa Dk. Ulimboka na Kibanda? Kama wameshindwa kazi kuna haja gani ya wao kuendelea kuwapo kazini wakati wananchi wanaishi kwa hofu ya kutekwa, kunyofolewa kucha, meno, kutobolewa macho na kutupwa msituni? Source:Tanzania Daima
HALI TETE: NANI ALIMTEKA DR ULIMBOKA????