Kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha San Francisco nchini marekani kumetokea ajali ya ndege iliyohusisha ndege moja ya Asian Airline ambayo iilkuwa na abiria wengi kutoka bara la Asia. Hadi ajali imetokea watu walioweza kujulikana uraia wao ni wachina 141 ambao kati ya kuna wanafunzi wa high school 32 wakitokea China kuelekea Marekani kwenye summer camp,abiria 77 ni wakorea,61 wamarekani,wahindi 2 na wengine. Watu karibia 180 wamekimbizwa hospitali baada ya kupata majeraha na waliofariki hadi sasa ni watu 2. Kutokana na maelezo ya maofisa wa Asian Airline, ndege yao haijapata crash hii kutokana tatizo la injini bali kuna tatizo lingine ambali bado halijajulikana kwa sababu hali ya hewa ilikuwa shwari kabisa. Kwenye mabaki ya ndege hiyo wataalamu wameweza kupata kifaa kinaitwa Black Box ambacho hurekodi mambo yote ya safari ya ndege, hivyo basi itasaidi katika kupata majibu juu ya sababu ya ajali hii