http://kariakoodsm.blogspot.com
KARIAKOO BLOG:Kwa Habari Kali Za Mjini | SIASA | BURUDANI | UCHUMI | FASHION | BLOGGER TRICKS | UDAKU | MICHEZO | WASILIANA NA MIMI|0713305567 |urassaombeni@yahoo.com|KWA| MATANGAZO| BABARI| USISITE PIA KUCOMMENT KWENYE HABARI ZETU | <div style='background-color: #de24de;'><a href='http://www.ikiloop.com/' title='link'></a></div>

Ujio wa Obama wazidi kutesa wakazi Dar



UJIO wa Rais wa Marekani, Barack Obama na viongozi wengine umezidi kuwa shubiri miongoni mwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumamosi umeonesha kwamba kwa siku kadhaa wananchi wamekuwa wakisumbuka kwenda makazini au kwenye shughuli zao nyingine kutokana na foleni kubwa wanazokumbana nazo barabarani, hivyo kuwalazimu baadhi yao kutembea kwa miguu.

Hali hiyo imesababisha adha kubwa pia kwa watu wenye magari binafsi, wanaolazimika kukaa muda mwingi njiani, hivyo kukwamisha shughuli zao.

Kumekuwa na msururu mrefu wa magari katika barabara nyingi ikiwemo ile ya Kilwa kutoka eneo la Bandari hadi Stesheni.

Mkazi mmoja, Onesmo Peter alisema ujio huo umeleta hasara kwa sababu umewafanya wakazi wengi kuchelewa kazini ama katika biashara zao.

“Nimetoka nyumbani eneo la Mtoni Mtongani majira ya saa 1.15 asubuhi na cha ajabu nikakwama katika eneo la Bandari kwa zaidi ya saa moja na nusu,” alisema Peter.

Dereva Juma Mtanda alilalamikia hali hiyo na kueleza kwamba kuwepo kwa foleni hizo kunatokana na miundombinu hafifu iliyopo na kuhoji sababu ya serikali kutotumia mbinu mbadala ya kuuwezesha ugeni huo kufika nchini bila kuathiri shughuli za wananchi wengine.

Neema Samora ambaye alishuka kwenye daladala akiwa na wenzake na kutembea kwa miguu ili kuwahi shughuli zake, alisema ujio wa Obama na viongozi wengine unawaweka katika wakati mgumu wa kuweza kukosa kazi kwani wengi wao hufanya kazi kama vibarua hivyo kuamua kushuka kwenye daladala na kutembea.

“Mimi binafsi leo nimeacha gari nyumbani na kulazimika kukodi pikipiki bila kupenda ili iniwahishe mjini kwani machungu niliyoyapata jana yametosha,” alisema Hadija Saidi mkazi wa Ukonga.

Amosi Petro alisema ikiwa kuna ugeni wowote unataka kuja nchini ni vyema serikali ikajipanga vizuri kuliko ilivyofanya sasa kwani kwa kiasi kikubwa imeathiri shughuli za wengine.

No comments:

Post a Comment

ShareThis